Ngassa aliyekuwa akiichezea Simba kwa mkopo kutoka Azam FC, amesaini
mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga lakini Simba wamesema
walishasaini naye mkataba wa mwaka mmoja.
Habari za uhakika kutoka
ndani ya Simba zimeeleza kuwa, Msimbazi wameamua kufanya mambo yao kimya
na wameamua kutumia mahakama ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine.
“Hakika
sasa tumeona suala hili si la kufanya kama filamu, maana wenzetu
(Yanga) pamoja na Ngassa wameamua kutufanyia uhuni. Wachezaji wanataka
kufanya Simba ni kama sehemu ya kuchota fedha na kuondoka.
“Kitu
kibaya zaidi tumegundua system (mfumo) ya soka imekuwa ikiwalinda sana
kutokana na ushabiki mkubwa uliopo katika kamati zilizo chini ya TFF.
Sasa sisi tumeona bora kuchukua hatua zaidi,” kilieleza chanzo cha
uhakika.
“Tutamfikisha Ngassa mahakamani, tutadai zaidi ya Sh milioni
200 kama sehemu ya kutaka fidia kutokana na mkataba tulioingia naye.
Mkataba upo, msione tumekaa kimya mnaona kama hatuna cha kusema.
“Ila
sasa tumeamua kufanya mambo kwa mfumo tofauti na leo (jana) usiku
tutakuwa na mkutano kwa ajili ya kujadili kuhusiana na suala hili na
tutajua lini rasmi apande kizimbani.”
Championi Jumatano ndiyo
lilikuwa la kwanza kuandika kuhusiana na Ngassa kusaini Yanga miaka
miwili na kueleza kila anachopata katika mkataba wake, achana na wale
waliosema katika stori yao eti anatarajia kusaini.
Kwa mujibu wa
chanzo hicho kutoka ndani ya Simba, mkataba kati ya Ngassa ulipelekwa na
kusajiliwa TFF tangu Desemba, mwaka jana.
Tayari baba yake amezungumzia kuhusiana na mwanaye kuhamahama na Yanga imeshatangaza
kumtambulisha kwa mashabiki Juni 3,,,,,Suala la Ngassa kutua Yanga limezua gumzo kubwa na huenda likazua mgogoro mkubwa baina ya timu hizo mbili.
Mwishoni
mwa mwaka jana, Ngassa alitua Simba kwa mkopo akitokea Azam, lakini
akakabidhiwa gari aina ya Toyota Verossa na Sh milioni 30 na Simba
kutangaza imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumalizika kwa
mkopo, lakini Ngassa mwenyewe amekuwa akisisitiza hana mkataba na
Msimbazi baada ya ule wa Azam kumalizika.
No comments:
Post a Comment