Friday, May 31, 2013

USHER AFUNGUKA KUHUSU MISUKUSUKO INAYOMWANDAMA JUSTIN BIEBER BIEBER

usher_grammy_engagement_rumouJustin-Bieber-Won-Billboard-Music-AwardsBaada ya msanii Justin Bieber kuwa katika vichwa vya habari vya media mbalimbali kwa matukio ambayo si mazuri katika siku za karibuni, Msanii wa Muziki Usher Raymond ambaye pia ni kaka mlezi na kiongozi wake, ameongelea swala hili na kusema kuwa anaelewa misukosuko ya Bieber kutokana na ukweli kuwa kwa sasa yupo katika umri wa mambo mengi wa ujana......Usher amesema kuwa, mtu yoyote angeweza kufanya kama Bieber ama hata zaidi katika umri kama ule na hatari zaidi, akiwa anafuatiliwa na mapaparazzi kwa karibu.
Bieber amekuwa mada ya majadiliano mbalimbali katika tasnia ya burudani hasa baada ya tukio la kuzomewa na mashabiki wakati akipokea tuzo za Billiboard, kulalamikiwa na majirani zake kwa uendeshaji mbovu wa magari na matukio mengine mengi yanayofanana na hili.

No comments:

Post a Comment