Taarifa za ujauzito wa pili wa Beyonce mwenye miaka 31 zimethibitishwa
jana May 17 na vyanzo tofauti na kuripotiwa na vyombo vingi vya habari
ikiwa ni siku chache toka acancel show yake ya Mrs Cartter World tour
huko Antwerp, Belgium kutokana na upungufu wa maji mwilini na uchovu
(dehydration and exhaustion).Tetesi za ujauzito wa pili wa Beyonce zimeunganishwa na maelezo aliyoitoa Bey mwenyewe katika mahojiano ya hivi karibuni na kituo cha ABC, “napenda kupata watoto zaidi, nadhani binti yangu anahitaji kupata company.”
Kwa kumbukumbu zetu, Jay na Beyonce ambao ni wa kwanza kuwa ‘billion dollar couple’ katika muziki imekuwa na kawaida ya kufanya mambo yao kwa usiri mkubwa hasa katika kipindi ambacho wanakuwa hawajaamua kuzifanya zijulikane.
Itakumbukwa wakati wanafunga ndoa iliwachukua muda mpaka watu kujua walifunga ndoa ya siri. Pia wakati wa siku za mwanzo za ujauzito wa Blue Ivy hawakuweza kuthibitika mapema kuwa Queen Bey alikuwa mjamzito, na baada ya Blue Ivy kuzaliwa haikuwa kazi rahisi kwa camera za mapaparazi kukiona kichanga chao mpaka muda ulipopita.

No comments:
Post a Comment