SAKATA la kijana Bonny Fabian Kavishe kudaiwa kumuua kwa kumpiga risasi
baba yake, mzee Livingstone Kavishe akiamini ni mwizi sasa ni simulizi
ya machozi kufuatia kusomwa kwa waraka mzito ulioandikwa na mtuhumiwa
huyo ambaye bado yupo mahabusu ya Polisi Mlandizi, Bagamoyo, Pwani.,,,,,Waraka huo ulizidi kuwatoa machozi baadhi ya waombolezaji siku ya
mazishi yaliyofanyika Marangu, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoa wa
Kilimanjaro kutokana na maneno yenye huruma ya Bonny kuomba msamaha.
WARAKA ULIANDIKIWA NDANI YA MAHABUSU
Habari zisizo na chenga wala
kumulika tochi zinasema, mtuhumiwa akiwa mahabusu aliamua kuandika
waraka huo na kumpa ndugu yake mmoja (jina halikupatikana) akimpa
maelekezo kwamba usomwe siku ya mazishi ya mzee huyo kabla hajafukiwa
kaburini kwa vile yeye hatakuwepo.
“Kwa kweli inauma sana! Jamaa
alipoona hatapata ruhusa ya askari ili akashiriki mazishi ya baba yake
aliomba karatasi na kalamu na kuandika waraka, akampa ndugu yake mmoja,
akamwambia usomwe siku ya mazishi ya marehemu kabla hajafukiwa
kaburini,” kilisema chanzo......MWILI WAAGWA NYUMBANI KWA MTUHUMIWA, WASAFIRISHWA NA WARAKA
Jumatano ya Mei 15, mwaka huu, mwili wa marehemu mzee Kavishe uliagwa
nyumbani kwa mtuhumiwa licha ya yeye kutokuwepo na ukasafirishwa kwenda
Marangu kwa mazishi.
Miongoni mwa mambo yaliyozingatiwa kwenye
kusafirisha mwili huo ni uwepo wa waraka huo ambao mtuhumiwa aliomba
usomwe mbele ya waombolezaji siku ya mazishi.
MANENO NDANI WARAKA NI HAYA
Siku ya mazishi, mwanaume aliyepewa
jukumu la kuongea kwa niaba ya familia aliusoma waraka huo huku
waombolezaji wakiwa makini kumsikiliza.
Alisema waraka huo
umeandikwa kwa mikono ya Bonny Kavishe, licha ya kuzungumzia mambo
mengine, aliwaomba msamaha ndugu, jamaa na marafiki kwamba wamsamehe kwa
kitendo cha kumuua baba yake.
Alisema alifanya kitendo hicho bila
kukusudia na wala hajui nini kiliendelea. Haikuwa nia yake kumtoa uhai
baba yake aliyefikia nyumbani kwake Mlandizi kwa ajili ya kusherehekea
harusi ya mdogo wa mtuhumiwa huyo iliyofanyika Mei 11, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment