Mwanadada mrembo na muigizaji wa bongo movies Jokate Mwegelo amabaye pia anamilki kampuni ya nywele iitwayo Kidoti, ameanzisha program iitwayo Kidotitime ikiwa na lengo la kusaidia wanafunzi kutambua na kukuza vipaji vyao wakiwa mashuleni. Akiandika kwenye ukurasa wake wa facebook na twitter mwanadada huyo alisema kuwa program hii itaingizwa katika shule zaidi ya ishirini na saba (27) kuanzia na mkoa wa Ruvuma- Songea na anaamini itakuwa na kuenea kwenye mashule mengine kwenye mikoa mbalimbali.
Katika ukurasa wake wa facebook jana aliandika:
“Jumamosi iliyopita nilikuwa kwetu songea vijijini kama mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa michezo ya Umisseta ngazi ya wilaya. Lakini vile vile nilipata nafasi kutambulisha program ya #KidotiTime itakatoingizwa kwenye ratiba za shule takribani 27 kwa kuanzia. Program hii ni kusaidia wanafunzi kujitahidi darasani huku wakigundua na kuendeleza vipaji vyao vingine. Sengwile”
Na kwenye ukurasa wa twitter aliandika
“Naanzisha kitu kinaitwa #KidotiTime kwenye shule 27 huku songea vijijini. Nashukuru walimu woooote kulipokea hili kwa moyo mmoja”
“#KidotiTime imeanza vijiji kutoa hamasa kwa watu wote kuwa hata huku kuna vipaji na vinafaa viendelezwe”
“#KidotiTime ni njia tu mmoja wapo ya kuvutia wanafunzi pia kufanya vizuri shuleni. Unaweza kuwa mwimbaji mzuri na kufanya vizuri darasani.”
Pia akiongea kwa simu na tovuti ya bongomovies.com meneja masoko wa kampuni ya Kidoti ndugu Peter Kasiga alisema kuwa Kidotitime ni moja ya shughuli mbalimbali za Kampuni ya kidoti katika kuboresha na kuendeleza vipaji na uwezo wa vijana nchini kote.
No comments:
Post a Comment