Monday, May 20, 2013

SIKU CHACHE TU BAADA YA KUTEMANA NA RIHANA, MAISHA YA CHRISS BROWN MATATANI, HIKI NDO KILICHOMPATA

chris grafitti-2
Kwa mujibu wa vyanzo, mwanasheria wa Chris, Mark Geragos alipokea simu kutoka kwa watu tofauti wasiojulikana wakitishia kumuua Chris Brown bila kutoa sababu. Baada ya vitisho hivyo Geragos aliamua kutoa taarifa idara ya polisi ya Los Angeles ambao wanaendelea kufanya upelelezi juu ya vitisho hivyo.
Hivi karibuni Chris Brown amekosa maelewano mazuri na majirani zake kutokana na wao kutofurahishwa na graffiti ya Chris aliyoichora nje ya uzio ya nyumba yake ya Hollywood Hills kwa madai kwamba kuna watoto wadogo ambao wanaishi na kupita eneo hilo ambao wanatishika na michoro hiyo yenye muonekano unaotisha, kitu ambacho kinahisiwa kuwa kinaweza kuwa moja ya sababu za vitisho alivyovipata.

No comments:

Post a Comment