Friday, May 17, 2013

VUNJA MBAVU ZA WAZIRI MAGUFULI BUNGENI DODOMA

WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli ndiye waziri namba moja hadi sasa kwa kulivunja mbavu Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma kutokana na vichekesho vyake wakati alipokuwa akijibu hoja za wabunge mbalimbali hivi karibuni.

Magufuli ambaye wengi humuita ‘Jembe’ kutokana na uchapa kazi wake, alikuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake na kuomba kuidhinishiwa Shilingi Trilioni 1.22 kwa mwaka wa fedha 2013/14.

No comments:

Post a Comment