Tuesday, May 28, 2013

NAMBA YA FREEMASON YAZUA HOFU!

HOFU imezuka nchini baada ya namba ya simu inayotajwa kuwa ni ya jamii ya watu wasiomwamini Mungu, Freemason kuhusishwa na umwagaji damu na kafara kutumika kuwapigia watu mbalimbali, Uwazi lina taarifa hii kwa ukamilifu.

Taarifa ambazo Uwazi limezipata, zinaeleza kwamba namba hiyo ni ya Freemason na kwamba, mpigiwaji akijaribu kupokea na kuzungumza, atakuwa ameunganishwa kwenye kafara hiyo.

Baada ya namba hiyo ya kutatanisha kuzuka na kuwapigia watu mbalimbali, inaelezwa kwamba iligundulika kuwa ni ya jamii hiyo na hivyo kusambazwa meseji ya kuwaonya watu wasipokee simu hiyo. NI NAMBA GANI?

Namba hiyo ni 0800226655 ambayo Uwazi limejiridhisha kuwa si namba ya mtandao wowote wa simu nchini wala nje ya mipaka ya Tanzania, maana hakuna namba kama hiyo

No comments:

Post a Comment