Funguka: Mambo vipi Profesa, nimekutafuta ili nipate msimamo wako kwenye bifu kati ya msanii mwenzako (Jide) na Ruge.
Profesa Jay: Kwanza nianze kusema kuwa mimi sina upande wowote ambao ninaweza kuusimamia, sipo kwa Ruge wala kwa Jide.
Funguka:
Kumekuwa na minong’ono mitaani kuwa upo upande wa Jide kwani mmekuwa
mkifanya kazi pamoja vilevile ni marafiki kwa muda mrefu na ndiyo maana
amekushirikisha kwenye wimbo wake wa Joto Hasira. Unalizungumziaje hili?
Profesa
Jay: Ishu siyo mimi kuwa upande wa Jide au wa Ruge, kitu ambacho
ninaweza kukizungumzia ni kwamba Jide alinishirikisha kwenye wimbo huo
hata kabla ya hilo bifu lao sijalifahamu. Mimi niliimba kutokana na
maudhui ya wimbo ulivyokuwa ukitaka. Kwa hiyo bado nasisitiza kuwa
sifungamani na upande wowote katika jambo hili.
Funguka: Kama ni hivyo, unachukuliaje suala la Jide na Ruge kufikia hatua ya kuburuzana mahakamani?
Profesa
Jay: Kuhusu hilo, sitakuwa msemaji sana ila kwa jinsi ninavyofahamu,
Jide ni msanii mkongwe. Kama unakumbuka nilishawahi kufanya naye traki
kadhaa kama Bongo Dar-es-salaam na Niamini. Kikubwa ni kwamba Jide
anajiheshimu sana na nadhani kila anachokifanya anakijua vizuri.
Funguka: Unamuongeleaje Ruge na uongozi mzima wa Clouds kuhusu sakata hili?
Profesa
Jay: Binafsi siwezi kuwaongelea Clouds au Ruge kwa jambo lolote, kwa
sababu ninaamini na wao ni watu wazima na wanafahamu nini
wanachokifanya.
Funguka: Hivi karibuni tumesikia wasanii kadhaa
wamejitoa kwenye orodha ya wasanii watakaomsapoti Jide kwenye shoo yake
ya Mei 31, vipi wewe utakamua kama kawaida?
Profesa Jay: Nikutoe
wasiwasi, mimi binafsi nitakuwepo kwenye shoo ya Jide na nitapiga mzigo
wa kufa mtu kumsapoti kwa akili yangu yote, nguvu zangu zote na moyo
wangu wote.
Funguka: Poa, nashukuru kwa ushirikiano wako, kazi njema.
Profesa Jay: Haina kwere.
No comments:
Post a Comment