Wednesday, May 22, 2013

KALI YA LEO: REAL MADRID WATELEKEZA BASI LAO LA KUSHEREHEKEA UBINGWA WA MFALME BAADA YA KUNYUKWA NA ATLETICO

Real Madrid walikuwa wakijiamini sana kuelekea fainali ya Ijumaa iliyopita ya Copa del Rey dhidi ya Atletico Madrid, lakini wapizani wao hao wakavunja uteja wa miaka 10 kwa kuwafunga Madrid na kubeba taji la kombe la mfalme.
Kutokana na kujiamini sana Madrid walikuwa wameshaandaa bus maalum kwa ajili ya kusherehekea ubingwa wao katika jiji la Madrid, lakini mambo yakawa tofauti wakafungwa na Atletico na matokeo yake wakaliacha bus lao la kusherehekea ubingwa likiwa tupu kwenye moja ya gareji moja iliyopo jijini humo.

Kwa upande wa Atletico wao wakalitumia bus lao kwa kutembeza kombe lao mbele ya maelfu ya washabiki ndani ya jiji la Madrid.

No comments:

Post a Comment