Powered By Blogger

Thursday, May 23, 2013

HIVI NDIVYO MCHUNGAJI ALIVYOFUMANIWA NA KUTEMBEZWA UCHI HADI KANISANI. SOMA HAPA

pasta afumaniwa Mtumishi mmoja wa Mungu amejikuta akipata aibu ya mwaka si tu mbele za Mungu bali hata kwa mkewe pamoja na mashuhuda wengine baada ya mkewe kumfumania ‘live’ kitandani akifanya mapenzi na mwana kwaya wa kanisa lake huko Kisumu nchini Kenya.,,,Habari zilizoripotiwa na mtandao wa Kenyan-Post zinasema msichana huyo mweye miaka 23 amekuwa na mahusiano ya muda mrefu na pasta huyo kabla hawajabambwa.
Kisa hiki ni kama movie ambazo tumezoea kuziona zenye story line ambayo unaweza kutabiri mwisho wake. Kwa mujibu wa mtandao huo, ile ‘siku ya 40’ mke wa pasta huyo alikuwa anatarajia kusafiri kwenda nyumbani kwao kusalimia wazazi wake hivyo mumewe alimsindikiza mpaka kituo cha basi, lakini alionekana kuwa mtu mwenye haraka na kumwambia mkewe kuwa siku hiyo ana mkutano muhimu hivyo anapaswa kuwahi. Baada ya kumfikisha kituoni aligeuza gari kwa haraka na kuondoka,
Huku nyuma mke wa pasta kwa bahati mbaya (upande wa pasta) na bahati nzuri (upande wake) aligundua kuwa amesahau zawadi aliyokuwa amemnunulia mama yake mzazi ambaye ndio anaenda kumsalimia hivyo ikabidi airudie nyumbani kisha asafiri na basi litakalokuwa linafuata.
Alipofika nyumbani anapoishi na mumewe alishangaa kukuta mlango haujafungwa kwa nje na huku anakumbuka walipoondoka waliufunga hivyo akahisi huenda wamevamiwa mchana kweupe, alipojaribu kuusukuma ulikuwa umefungwa kwa ndani ndipo alipoomba msaada wa majirani wakavunja kitasa na kuingia ndani.
Mama huyo alipigwa na butwaa kwa kile alichokikuta ndani baada ya kumkuta msichana anayemfahamu kuwa kiongozi wa kwaya ya kanisani la mumewe wakiwa uchi wa mnyama katika kitanda chake na mumewe.
Maamuzi aliyochukua ni kuwavamia kitandani na kuzitupa nje kupitia dirishani nguo zao wote lakini kwa bahati mbaya msichana aliyemfumania alifanikiwa kukimbia na kumuacha pasta mwenyewe.
Huwa wanasema hasira ni hasara na maamuzi ya hasira hugeuka majuto baadae, baada ya mmbaya wake kukimbia aliamua kumvuta mumewe (pasta) akiwa uchi wa mnyama na kumtembeza mbele ya umati wa watu mpaka katika kanisa analotoa huduma pasta huyo kwa lengo la kufichua mabaya yake.
Bahati nzuri alijitokeza mwanaume mmoja aliempatia shati lake ili ajisitiri.

No comments:

Post a Comment