Saturday, May 18, 2013

MAGUFURI AGEUKA JOTI BUNGENI, HIVI NI BAADHI YA VICHEKESHO ALIVYOTOA BUNGENI. SOMA HAPA

Mheshimiwa huyo alimudu kuwafanya waheshimiwa wacheke sana huku ujumbe ukifika tofauti na mawaziri wengine waliopita ambao hotuba zao zinadaiwa kuwa zilijaa ushawishi wa usingizi.
“Tunajenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Dodoma kwenda Iringa, wale watani zangu wa Iringa hawatakuwa na haja ya kujinyonga kwenye miti, sasa watakuwa wakilala barabarani tu.”
Wabunge walivunjika mbavu kwa vicheko. Watani zake alimaanisha Wahehe ambao inadaiwa wanapokuwa na hasira wana tabia ya kujiua kwa kujinyonga (ni madai).
Kama vile haitoshi, waziri huyo akijibu swali la Mbunge wa Same Mashariki, Mheshimiwa Anne Kilango Malecela kuhusu barabara inayopita kwenye Kiwanda cha Tangawizi kupewa hadhi, pia alitumbukiza utani.
“Mheshimiwa Anne Kilango yale uliyosema tunayafanyia kazi, kuhusu barabara inayopita Kiwanda cha Tangawizi kupewa hadhi tumepokea, maana pia mheshimiwa rais alitupa maagizo.
“Nimeamini una akili sana ndiyo maana mtani wangu Malecela alitoka Dodoma na kwenda milimani Same huko, kwa nini hakuja usukumani?”
Aidha, waziri huyo akimjibu Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ambaye alitoa ushauri kwa Wizara ya Ujenzi kupunguza idadi ya miradi na kukamilisha mmoja baada ya mwingine ili wizara iweze kufanikiwa huku akilalamikia kutojengewa barabara jimboni kwake, Magufuli aliwavunja mbavu tena wabunge:
“…ushauri wako ni mzuri ndiyo maana wizara yangu imeamua kuacha kujenga barabara jimboni kwako ili tukamilishe sehemu nyingine kwanza…”
Hata hivyo, wakati wabunge wakivunjika mbavu, Magufuli alisema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) haina ubaguzi na itajenga barabara hiyo iliyoko jimboni kwa mbunge huyo.
Akimjibu Mbunge wa Viti Maalum (CCM –Bunda), Ester Bulaya ambaye alisema kwamba anamkubali waziri huyo kutokana na utendaji wake, Magufuli naye alisimama na kusema:
“Hata mimi namkubali Ester Bulaya...”
Aidha, Magufuli aliwashangaa wabunge wa upinzani ambao walionesha kutaka kumpinga na kuwaambia kuwa bosi wao, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alionesha kumkubali na kuzimwagia sifa sera za CCM baada ya kukamilishiwa barabara iliyoko jimboni kwake Hai, Kilimanjaro.
“Kama kuna mtu anabisha ushahidi uko hapa aje nimuoneshe, mheshimiwa aliandika kwenye mtandao (akautaja jina zima) kisha akasema kama mtu haamini akatoa flashi yenye sauti aliyodai ni ya Mbowe.
VIDOKEZO VINGINE:
Alimwambia mbunge wa upinzani ana moyo wa CCM CCM, amekaa ki-CCMCCM.
Katika kutekeleza uvunjaji wa nyumba zilizoingilia hifadhi ya barabara aliwahi kuvunja ukuta wa nyumba ya baba yake mzazi.

No comments:

Post a Comment