Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu iliyotumwa kwa vyombo vya 
habari juzi, ilifafanua kwamba Rais Kikwete hafahamu kuwepo mipango 
hiyo, na kumtaka Profesa Lipumba aisaidie jamii kusema nani anafanya 
mpango huo, ili ukweli ujulikane.
“Aidha, Mheshimiwa Rais anawasihi wanasiasa na Watanzania kwa ujumla, 
kuacha tabia za uongo na uzushi na kuwapotezea muda Watanzania kufikiria
 mambo yasiyokuwepo.
“Ukweli ni kwamba, kama ambavyo amesema mara nyingi, ni matarajio ya 
Rais Kikwete kuwa mchakato wa Katiba utakamilika mwaka 2014, na 
kuwezesha Uchaguzi Mkuu wa 2015 kufanyika chini ya Katiba Mpya kama 
inavyotarajiwa ,” ilieleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Ikulu, Rais Kikwete anatarajia baada ya uchaguzi wa 2015, 
atapata nafasi ya kustaafu mwisho wa kipindi chake cha uongozi kwa taifa
 letu.


 
No comments:
Post a Comment