Tuesday, May 28, 2013

MAMA NGWAIR: MWANANGU ALINIAHIDI KURUDI IJUMAA ILIYOPITA

Akiongea kupitia kipindi cha Amplifire cha Clouds FM, kutoka mkoani Morogoro, mama mzazi wa msanii Albert Mangwair aliyefariki dunia leo akiwa nchini Afrika Kusini, amesema kuwa mara ya mwisho kuwasiliana na marehemu ilikuwa wiki mbili zilizopita ambapo Mangwair alimwambia kuwa mzima na anaendelea vizuri na kwamba angerejea nchini Ijumaa iliyopita. Aliongeza kuwa taarifa za kifo cha mwanaye amezipata jioni hii kwa masikitiko. Wakati Mangwair anaelekea Afrika Kusini hakumuaga mama yake japo akiwa huko alikuwa anawasiliana naye. Kuhusu taarifa za mazishi mama Mangwair amesema bado anasubiri shemeji zake wafike ili wapange

No comments:

Post a Comment