Friday, May 17, 2013

LINAH & BARNABA HUENDA WAKATUPIWA VIRAGO THT BAADA YA SAKATA LA JIDE. MKASA KAMILI HUU HAPA

KUELEKEA shoo maalumu ya Miaka 13, ya mwanamuziki nguli wa bongo fleva nchini na kiongozi wa bendi yenye msisimko mkubwa ya ‘Machozi Band’, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ au Jide’  huenda kwa upande wa wasanii wa Nyumba ya Vipaji ya THT, Linah Sanga na Barnaba  mwaka huu ukawa mchungu kwao kufuatia kuwepo taarifa za kutimuliwa na uongozi wa juu.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka kwa mtu wa karibu wa Linah kilieleza kuwa mpaka sasa msanii huyo hana raha na wala hajui ataanza vipi katika harakati zake za kimuziki hasa kufuatia hivi karibuni kukacha shoo ya nguli Lady Jay Dee kwa shinikizo kutoka kwa wakubwa zake.

Hata hivyo, Linah inadaiwa uongozi wa juu umekaa kikao na hatua iliyofuatia kwenye kikao hicho ni kuwaondoa kabisa kwani huenda wakatia doa wasanii wenzao ndani ya kundi hilo.

No comments:

Post a Comment