Saturday, May 11, 2013

WATAPELIWA KWA KUCHIMBA KABURI

KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Kesi Dikoroma na dada mmoja (jina halikupatikana mara moja) wamejikuta wakitapeliwa simu zao baada ya kupewa tenda ya kuchimba kaburi.

Wawili hao wamekutwa na mkasa huo hivi karibuni katika makaburi ya Ulongoni, Tabata-Segerea, jijini Dar, ambapo imeelezwa kuwa, Kesi ambaye hufanya shughuli za kuchimba makaburi, alipatwa na msala huo baada ya baba mmoja ambaye hakufahamika jina lake kufika makaburini hapo na kuwapa tenda feki ya kuchimba kaburi.

“Aliwaambia kuwa ana shida ya kuchimbiwa kaburi litakalogharimu shilingi laki tano na kudai anataka baada ya kuchimbwa lijengwe kabisa.

“Ndipo Kesi na huyo dada ambaye alipewa tenda ya kuchota maji, waliingia mzigoni huku mwingine akaambiwa akalete matofali na marumaru. …

No comments:

Post a Comment