Monday, May 13, 2013

WASANII WA KAOLE WAPATA AJALI

WASANII wa Kundi la Kaole, Mariamu Athuman ‘Kalunde’ na Herry Mohamed ‘Niko’ wamepata ajali na kuumia vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi na kuacha njia.

Ajali hiyo ilitokea hivi karibuni maeneo ya Kiteto mkoani Manyara ambapo wasanii hao ambao ni wapenzi, walikuwa wakitumia gari aina ya Vogue wakielekea kwenye msiba. Walikuwa watu watano kwenye gari hilo ambao wote walijeruhiwa sehemu mbalimbali.

No comments:

Post a Comment