Powered By Blogger

Thursday, May 16, 2013

DIAMOND ATOA USIHA KWA MASHABIKI WAKE DUNIANI KOTE....!!

Ni siku nyingine tena napenda kumshukuru mwenyezi
Mungu mwingi wa rehema zake kwa sisi wanadamu......
sote kwa ujumla,wewe unaesoma ujumbe huu na ata
 ambae yupo miangaikoni mungu amfanyie wepesi......Binafsi
Mi mzima kabisa wa afya tele pamoja na 

Familia yangu nzima kwa ujumla.....Namshukuru 
sana Mungu kwa Pumzi yake ya bure
kwetu na kuzidi kunibariki na kunifungulia milango ya
Baraka kwenye kazi 
yangu ya Muziki ....Si kama sisi tuliopo
 hapa wazima ni wema sana machoni pakee lakini kwa
kudra zake mwenyezi Mungu Tu angali wazima wa Afya....!!
Nachukua nafasi hii kuwashukuru Mashabiki zangu kote
Nchini na hata nje ya nchi na Dunia nzima kwa support
 yenu kwangu na mapenzi yenu kwangu ya dhati.....!!
Hakuna Nyota Bila Shabiki Bila Nyinyi mi si chochote.....!!
Binafsi Nafurahi sana kuwa karibu na nyie
japokuwa sio wote ntakaowaridhisha kwa ujumla
kwa kuwa ni mashabiki wengi sana kila kona na pembe ya Dunia.....
Lakini Mda huu mdogo naopata nafurahi kuwajulia
hali kwa pamoja.....

Cha Msingi napenda kuwatakia mafanikio na baraka tele
juu yenu iwe kwenye masomo,Biashara,kazi hata kwa wale wagonjwa,wasiojiweza na vilema 

Mkono wa Mungu
 ukawe Juu yenu kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwingi wa
 baraka na daima utuwazia Mema Juu yetu hata
kwa mabaya mengi tumkoseayo...!!
Upendo na Amani daima utawale kati yenu katika Maendeleo
ya kujenga taifa letu kwa nguvu na umoja kama Nguzo ya
Muunganiko na umoja kati yetu.....Dini wala ukabila usiruhusu
vitawale kati yenu na kujenga chuki mioyoni

 mwenu kutokana na tamaa za baadhi ya watu 
kusababisha mtafaruku kati yetu
viumbe wa Mungu....!!
Mshukuru Mungu kwa hapo ulipo.....Hakuna kitu
kibaya kama kutokuamini wewe si
 chochote wala si lolote.....
Amini ya kwamba upo dunia kwa makusudi ya
mwenyezi mungu na Mungu anakusudi na
wewe hapo ulipo......!!!
Napenda kuwatakia Jioni Njema.....Ni Hayo Tu
    kwa Leo....NAWAPENDA SANA......................................!!!!!!!

No comments:

Post a Comment