Sunday, May 12, 2013

CLOUDS WAMPELEKA LADY JAYDEE MAHAKAMANI

Taarifa zilizotufikia ambazo bado zipo chini ya kapeti ni kwamba Kampuni ya Clouds Media Group, imeamua kumfungilia mashitaka msanii nguli wa Bongo Fleva na kiongozi wa bendi ya Machozi, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’. Clouds imeamua kufungua mashitaka hayo baada ya Lady Jaydee kuwachafua viongozi wawili wa juu wa kampuni hiyo ambao ni Mkurugenzi Mtendaji , Joseph Kusaga na  Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo, Ruge Mutahaba katika mitandao ya kijamii hivi karibuni. Lady Jaydee anatakiwa kuripoti katika Mahakama ya Kinondoni kukabiliana na tuhuma hizo.

No comments:

Post a Comment