Powered By Blogger

Saturday, June 1, 2013

OBAMA ATUMIWA BARUA NYINGINE YENYE SUMU HATARI AINA YA RICING.SOMA HAPA

ObamaRicin

Shirika la upelelezi la Marekani FBI limesema kuwa barua yenye sumu hatari aina ya ricing imetumwa kwa rais Barack Obama kutoka Spokane katika jimbo la Washington, siku ambayo barua ya sumu kama hiyo ilipotumwa kwa Jaji wa mahakama kuu na kwa posta.

Mtu mmoja alikamatwa wiki iliyopita huko Spokane kuhusiana na barua hiyo iliyotumwa kwa jaji na ambayo ilizuiliwa tarehe 14 mwezi huu.

FBI imesema barua iliyokuwa imetumwa kwa rais Obama iligunduliwa tarehe 22 na kuongeza kuwa barua nyingine kama hiyo ilikuwa imetumwa kwenye kituo cha ndege za kijeshi kilicho karibu.

Taarifa ya FBI na ya huduma za posta imesema kuwa barua zote 4 ziliwekewa stampu tarehe 13 Mei huko Spokane.

Tatu kati ya barua hizo zimethibitishwa kuwa na sumu ya ricin na nyingine moja bado inachunguzwa.

No comments:

Post a Comment