
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameibuka na kuelezea
kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake zilipendwa, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
ambaye ni mwigizaji na modo moto wa kuotea mbali Tanzania
Akizungumza kwa uhakika kabisa, Diamond alisema inampasa amuombe radhi
Jokate kwa sababu katika uhusiano wao, Jokate hakuwahi kumkosea ila yeye
ndiye tatizo na chanzo cha kuachana kwao.
DIAMOND ANAFAFANUA
“Inanipasa nimuombe radhi Jokate. Ni kweli nilimtenda vibaya wakati wa
mapenzi yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi kufanya jambo lolote
kinyume. Sijui niseme nini lakini nataka kueleza wazi kuwa mimi ndiyo
sababu ya kuachana kwetu na ilitokea tu.
“Naamini hilo jambo lilimuuma sana, maana nakumbuka wakati ule, baada ya
mimi kurudi kwa Wema (Sepetu), watu walimwandama sana kwa maneno na
alionekana msaliti lakini ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini ndiyo
hivyo, siwezi kufafanua zaidi.
“Kutoka moyoni mwangu, namuomba msamaha Jokate, kama hatanisamehe
nitaendelea kumuomba mpaka naingia kaburini. Sina raha kabisa kutokana
na jambo hilo. Lazima niwe mkweli.”
JACQUELINE WOLPER
Diamond alikwenda mbali zaidi na kuwazungumzia baadhi ya wasichana
aliowahi kutoka nao kimapenzi akiwemo mwigizaji Jacqueline Wolper
ambaye alisema ni mwanamke aliyempenda sana, ndiyo maana alimtungia
wimbo wa Mawazo.
PENNY SASA
Kwa upande wa mpenzi aliye naye sasa, Mtangazaji wa Runinga ya DTV,
Penieli Mungilwa ‘Penny’ alisema ni mwanamke mtulivu na sahihi kwake kwa
sababu anatambua majukumu yake kwake, pia anamheshimu.
“Huyu kwa kweli ana karibu sifa zote alizonazo Wema ila uzuri wa Penny
ananiheshimu sana. Hafanyi mambo yake hadharani. Unajua wakati nikiwa na
Wema hata kama akifanya mambo yake siku mbili au tatu baadaye nayaona
kwenye magazeti, tofauti na Penny ambaye kwangu mimi naona ananiheshimu,
hata kama anafanya mambo yake ni kwa
siri.